ALIYEKUWA rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kati ya tarehe 7 Aprili 1972 hadi 30 Januari 1984, Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia leo mchana nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Saalam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kimethibitishwa na mmoja wa wanafamilia ya marehemu na anatarajiwa kuzikwa kesho Kisiwani Zanzibar.
Marehemu Jumbe atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuiongoza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar akichukua nafasi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu Abeid Aman Karume aliyefariki mwaka 1972.
Enzi za uhai wake akiwa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar alishirikiana na rais wa wakati huo wa Tanzania na mwenyekiti wa chama cha TANU hayati Julius Nyerere kuanzisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvunja vyama vya TANU na ASP na kuunda chama kimoja cha CCM.
Enzi za uhai wake Alhaji Jumbe aliwahi kutoa wosia wake hadharani akitaka mazishi yake yasibebe sura ya kitaifa na wala jeneza lake lisifunikwe bendera ya taifa au ya chama na kuomba yawe ya mazishi ya Muislamu na mwananchi wa kawaida.
Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa rais wa pili wa Zanzibar toka mwaka 1972 hadi 1984 alipojiuzulu. Aboud Jumbe alizaliwa mwaka 1920 huko kisiwani Zanzibar ( Tanzania ).
Alitanguliwa na Abeid Amani Karume Makamu wa Rais wa Tanzania1972-1984 akafuatiwa na
Ali Hassan Mwinyi
#Kauli_ya_Zitto_Kabwe baada ya kupata taarifa ya kifo cha Alhaji Jumbe
"Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ametangulia mbele ya Haki. Inna lillah waina ilaih raajiun.
Mzee Jumbe atakumbukwa katika historia ya Tanzania Kama Kiongozi aliyeamini na kusimamia anachoamini bila kujali madhara yake. Alipoteza nafasi zake za Uongozi Kwa sababu ya msimamo wake kuhusu muundo wa Muungano kutoka Serikali 2 kwenda Serikali 3.
Mzee Jumbe ameacha maandiko kupitia kitabu chake cha The Partnership ambacho ndugu yetu Ali Ally Saleh ' Alberto ' alipata heshima ya kukifasiri.
Pia Mzee Jumbe ameacha ' memoir ' yake ambayo ninaamini walioachiwa sasa wataweza kuitoa ili dunia ipate kujua mengi ambayo labda hatujui kuhusu Nchi yetu.
Hivi hapa Tanzania kuna Hata barabara yenye jina la Aboud Jumbe Mwinyi? Daraja? Nchi hii wakubwa wakigombana huwa hawasameheani?
Wazanzibari wanaweza kutumia msiba wa Mzee Jumbe kujenga maridhiano na kuanza kujenga Zanzibar kwa pamoja?"-Zitto Kabwe.

Social Plugin