Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tundu Lissu Afikishwa Mahakamani ..Asomewa Mashtaka Matatu





HATIMAYE Jeshi la Polisi Jijini Dar es salaam limemfikisha rasmi kizimbani Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo Singida Mashariki wilaya ya Ikungi mkoani Singida.


Tundu Lissu ambaye alikamatwa Juzi mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara Ikungi, Singida na kusafirishwa usiku, kulazwa Chamwino Dodoma na kufikishwa Dar jana saa saba mchana alilazwa rumande kabla ya kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana wa leo.

Akionekana mwenye kujiamini, Lissu amewasili Mahakamani Kisutu akitokea mahabusu ya Kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam saa nane na dakika arobaini na nane (14:48) akiwa kwenye gari yenye namba za usajili T 517 BET Corolla na akisindikizwa na ulinzi mkali wa jeshi la polisi.


Lissu ameshtakiwa kwa makosa matatu la kwanza kutoaa maneno ya uchochezi kwamba Agosti 2 katika Mahakama ya Kisutu kwa nia ya kujenga chuki kwa wananchi dhidi ya Rais na Serikali alitoa maneno ya uchochezi.

Shtaka la pili pia uchochezi kwamba Agosti 2 katika mahakama hiyohiyo kwa nia ya kudharau mhimili wa utoaji haki, alisema kuwa hawezi kufungwa kwa mashtaka na kesi ya upuuzi na shtaka la tatu ni la kudharau mahakama akidaiwa kuwa tarehe hiyohiyo mahakamani hapo, alitoa maneno ya uchochezi kuwa hawezi kufungwa kwa kesi na mashtaka ambayo ni upuuzi na ya kimagufulimagufuli

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com