Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo Agosti 5 2016 limechezesha droo ya mechi za play offs kwa ajili ya mechi za Ligi ya Europa League, UEFA limechezesha droo ya mechi za play offs kuelekea michuano ya Europa League hatua ya makundi, mechi za kwanza zitachezwa August 18 na marudiano itakuwa Agosti 25.
Kwa upande wa KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta imepangwa na klabu ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia na mchezo wa kwanza watacheza ugenini na wakifanikiwa kuitoa timu hiyo ni rasmi Genk itakuwa imefuzu katika hatua ya makundi, Lokomotiva ilimaliza nafasi ya nne Ligi Kuu Croatia msimu 2015/2016.
KRC Genk ya Samatta itakuwa inasubiri droo itakayochezeshwa August 26 Monaco Ufaransa na kusubiri itapangwa na vigogo gani hiyo kama itafanikiwa kuitoa Lokomotiva, miongoni mwa vigogo vitavyashiriki Europa League ni Man United ambapo wameanza hatua ya makundi moja kwa moja.
RATIBA YA MCHUJO WA MWISHO WA EUROPA LEAGUE KABLA YA HATUA YA MAKUNDI
Astana (KAZ) v BATE Borisov (BLR)
AEK Larnaca (CYP) v Slovan Liberec (CZE)
Arouca (POR) v Olympiacos (GRE)
Dinamo Tbilisi (GEO) v PAOK (GRE)
Midtjylland (DEN) v Osmanlıspor (TUR)
Austria Wien (AUT) v Rosenborg (NOR)
Trenčín (SVK) v Rapid Wien (AUT)
Beitar Jerusalem (ISR) v Saint-Étienne (FRA)
Lokomotiva Zagreb (CRO) v Genk (BEL)
Vojvodina (SRB) v AZ Alkmaar (NED)
Maribor (SVN) v Qäbälä (AZE)
Gent (BEL) v Shkëndija (MKD)
Slavia Praha (CZE) v Anderlecht (BEL)
İstanbul Başakşehir (TUR) v Shakhtar Donetsk (UKR)
Astra Giurgiu (ROU) v West Ham United (ENG)
SønderjyskE (DEN) v Sparta Praha (CZE)
Fenerbahçe (TUR) v Grasshoppers (SUI)
Sassuolo (ITA) v Crvena zvezda (SRB)
Brøndby (DEN) v Panathinaikos (GRE)
IFK Göteborg (SWE) v Qarabağ (AZE)
Krasnodar (RUS) v Partizani Tirana (ALB)
Maccabi Tel-Aviv (ISR) v Hajduk Split (CRO)
Social Plugin