Mauaji ya vikongwe yameendelea kujitokeza mkoani Shinyanga ambapo katika kipindi cha Mwezi Januari mwaka 2015 hadi mwezi Agosti mwaka 2016 Vikongwe 26 kwa kile kilichodaiwa kujihusisha na vitendo vya kishirikina huku viongozi wa madhehebu ya dini wakiitupia lawama serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kutowapa ushirikiano ikiwemo kupiga vita mauaji.Anaripoti mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde .
Akizungumzia hali ya amani mkoani Shinyanga, katika kikao cha viongozi wa dini kilichoitishwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alisema bado kuna tatizo la mauaji ya vikongwe mkoani humo.
Muliro alisema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba mwaka 2015 jumla ya vikongwe 20 waliuawa kutokana na imani za kishirikiana ambapo kati yao 15 ni kutoka wilaya ya Shinyanga,watatu kutoka wilaya ya Kishapu na wawili kutoka wilaya ya Kahama.
Alibainisha kuwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti mwaka 2016 vikongwe sita wameuawa mkoani Shinyanga kati yao watatu kutoka wilaya ya Shinyanga na wengine watatu kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Muliro aliwataka wadau wote wa amani kujitokeza kupiga vita mauaji ya vikongwe kwani yanatia doa mkoa na taifa kwa ujumla na kwamba jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kuwasaka na kuwakamata kisha kuwafikisha mahakamani waganga wa jadi wanaodaiwa kuchangia mauaji hayo kutokana na ramli chonganishi.
“Tumejitahidi kumaliza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi,hili la mauaji ya mama na bibi zetu ni tatizo kubwa,ni aibu sana kuua mama aliyekuzaa na kukulea”,aliongeza Muliro.
Wakichangia hoja katika kikao hicho ,asilimia kuwa ya viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Shinyanga waliitupia lawama serikali mkoani humo kwa kutowashirikisha katika masuala mbalimbali , badala yake wanasubiri mpaka unapotokea ugeni wa viongozi wa kitaifa hali ambayo imekuwa ikichangia kuongezeka kwa vitendo viovu yakiwemo mauaji ya vikongwe.
Walisema hivi sasa kuna ukuta kati ya viongozi wa dini na serikali ya mkoa wa Shinyanga kwani wamekosa ushirikiano katika masuala mbalimbali mfano wanapowapa mialiko mara nyingi wamekuwa hawajitokezi na badala yake viongozi wa serikali wamekuwa wakiwakumbuka viongozi wa dini katika baadhi ya matukio tu kama vile kutambulishwa kwa wageni wanaofika katika mkoa.
Sheikh mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya alisema tatizo la mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina linaendelea kujitokeza kutokana na viongozi wa serikali kutoshirikiana na viongozi wa dini kupiga vita mauaji hayo ambayo yanakatili uhai wa watu wasiokuwa na hatia.
“Ulipokesekana ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na dini kumechangia kutokea mauaji mengi inasikitisha sana kuona vikongwe 26 wameuawa kuanzia mwaka jana 2015 mpaka sasa ,mambo haya yatakoma iwapo viongozi wa dini tutapewa ushirikiano na serikali kwani yapo mambo ambayo serikali pekee haiwezi kuyafanya,kipindi cha mauaji ya albino viongozi wa dini tulishirikishwa lakini sasa ushirikiano umelegalega‘’alisema sheikh Makusanya.
Aliwataka viongozi wa serikali kubadilika na kudumisha ushirikiano ambao utasaidia kukabiliana na changamoto zilizopo yakiwemo mauaji ya vikongwe,watu wenye ualbino na tatizo la ajali za barabarani ambalo linaongezeka kwa kasi ndani ya mkoa huo.
“Viongozi wa serikali wamekuwa wakitukumbuka pindi yanapotokea matukio tu ama pale wanapokuja wageni katika mkoa wetu, naamini tukiungana pamoja katika hili itasaidia sana kumaliza tatizo la mauaji ya vikongwe”,aliongeza Sheikh Makusanya.
Sheikh Makusanya alishauri pengine viongozi wa serikali wanapoenda maeneo ya vijijini ambako matukio mengi hutokea waambatane na viongozi wa dini ili washiriki kuwapa elimu wananchi ili wawe na hofu ya mungu waache kutenda uovu na hatimaye kuondokana na mauaji ya vikongwe ambayo ni chukizo kubwa mbele ya mwenyezi mungu.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Dayosisi ya Shinyanga, Dkt. John Nkola aliitaka serikali kufanya utafiti wa kina ili kujua kiini cha mauaji ya vikongwe ambayo yamekuwa ya kihistoria katika mkoa wa Shinyanga.
“Naomba serikali itafute wadau wafanye utafiti ili kubaini chanzo haswa cha mauaji haya,haiwezekani mkoa uendelee kuwa na sifa mbaya,hapa kuna tatizo lazima tubaini kiini cha mauaji ya ndugu zetu hawa kwani na sisi ni wazee watarajiwa”,aliongeza Askofu Nkola.
Awali akifungua kikao hicho mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack aliweka wazi kuwa hakuwaita viongozi hao ili kuwapa maelekezo bali kujadili changamoto zilizopo yakiwemo mauaji ya vikongwe,albino na jinsi ya kupunguza matukio ya ajali ambazo zinaendelea kutokea maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Shinyanga wakiwa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga jana Agosti 25,2016
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumzia hali ya amani katika mkoa wa Shinyanga ambapo alisema tatizo kubwa sasa ni ajali za barabarani hususani za pikipiki na baiskeli sambamba na mauaji ya vikongwe yanatokana na imani za kishirikina
Viongozi wa dini wakiwa ukumbini
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ,ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza ukumbini
Viongozi wa madhehebu ya dini wakiwa ukumbini
Kamanda Muliro akisisitiza umuhimu wa wadau wote wa amani kushirikiana katika kulinda amani ya nchi
Viongozi wa madhehebu ya dini mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga Shaaban Luseza akichangia hoja ukumbini ambapo alisema matukio mengi ya uovu/uhalifu yanatokana na binadamu kukosa hofu ya mungu hivyo kuwasisitiza viongozi wa dini kuhakikisha wanafikisha elimu ya dini katika maeneo ya vijijini ambako ndiko mauaji ya vikongwe yanatokea badala ya kujikita mjini tu
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi wa dini wakiwa ukumbini
Sheikh mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akiachangia mada ukumbini ambapo alisema mauaji ya vikongwe yanazidi kujitokeza kutokana na viongozi wa serikali kutowashirikisha viongozi wa dini hivyo kuwataka kubadilika ikibidi wawe wanaambatana kwenda kwa wananchi kuhubiri amani
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala akizungumza ukumbini ambapo aliwahamasisha watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi
Kikao kinaendelea
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Dayosisi ya Shinyanga, Dkt.John Nkola akizungumza ukumbini ambapo alisema ni vyema sasa ukafanyika utafiti ili kubaini kiini cha mauaji ya vikongwe huku akihamasisha wananchi kupiga vitendo vyote vinavyoweza kusababisha amani ya nchi kutoweka
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifunga kikao hicho..Kulia kwake ni Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Social Plugin