Wauguzi Wawili na Askari 1 wa JWTZ Wakamatwa na Vyeti Feki 690 Vya Kutolea Huduma za Kutibu Binadamu


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma ,DCP Ferdinand Mtui akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake(hawapopichani),mbele yake ni vyeti feki na vifaa mbalimbali vilivyokuwa vinatumika kutengenezea vyeti hivyo -Picha na Rhoda Ezekiel Malunde1 blog Kigoma

Vyeti vya kughushi vikiwa vimekamilika kwa ajili ya kutumika kuombea kazi katika maduka ya dawa na vituo vya afya/hospitali

Vyeti feki vikiwa tayari kwa ajili ya matumizi

Vyeti vikiendelea kutengenezwa steshenari ya Upendo Kigoma

Zoezi la kutengeneza vyeki feki likiendelea
******

Watu watano wakiwem wauguzi wawili wa hospitali ya mkoa Maweni na afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za vyeti 690 vya kugushi vya taaluma ya afya kwa ajili ya kuuza vyeti kwa watu wengine ili wavitumie kuomba kazi maeneo mbalimbali nchini. Mwandishi wa Malunde1 blog mkoani Kigoma Rhoda Ezekiel,anaripoti.


Baadhi ya vyeti vimekutwa vikiwa vimekamilika kwa majina na vingine vikiwa vinaendelea kutengenezwa katika steshenari ya Upendo iliyopo katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma kwa lengo la kuvitumia kuombea kazi katika vituo vya afya na maduka ya dawa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa wa polisi mkoa wa Kigoma, DCP Ferdinand Mtui alisema askari wakiwa na wataalamu kutoka baraza la Famasia walianza msako sehemu mbalimbali za mkoa huo ambapo Agosti 9 mwaka huu walimkamata Dickson Mshahilizi (47) ambaye ni muuguzi katika hospitali ya rufaaa ya Maweni.

Alisema askari walifanya upekuzi kwenye nyumba yake na kukuta vyeti mbalimbali vya kutolea huduma za dawa za kutibu binadamu katika maduka ya dawa .

Mtui alisema vitu vingine vilivyokamatwa nyumbani kwa mtuhumiwa ni pamoja na vyeti 90 vya Nursing Assistance ,Laboratory Attendant vyeti 37, Dispensing tisa vyeti hivyo vikiwa vimekamilika.

Vingine ambavyo vilikuwa havijakamilika ni vyeti 667 vya Nursing Assistance ,Laboratory attendant vyeti 126 pamoja na kifurushi kimoja chenye vivuli vya vyeti mbalimbali na bahasha yenye paspoti ,madaftari 12 yenye orodha ya majina ya watu mbalimbali na mihuri ya vyuo mbalimbali vya Nursing ,wakuu wa vyuo na waganga wakuu wa mikoa ya Kigoma, Kagera,Singida ,Mwanza na Tabora.


Aliongeza kuwa katika msako huo askari walimkamata Zawadi James (42) ambaye pia ni muuguzi katika kituo cha Afya cha Ujiji mkazi wa Kazegunga Mkoani humo kwa kosa la kukutwa na vyeti vitatu vya Wauguzi wasaidizi,kabuuleta moja ya pikipiki na nyundo moja vinavyotumika kutengeneza mfano wa mihuri ya moto.

Kamanda Mtui aliongeza kuwa Agosti 10,mwaka huu, askari wakishirikiana na Baraza la famasia walifika katika steshenari iitwayo Upendo eneo la Mwanga Kigoma na kukutwa steshenari inatumika kutengeneza vyeti vya kugushi na kukamata kompyuta mpakato aina ya Toshiba ikiwa na soft copy ya vyeti vya vyuo mbalimbali vya Afya vilivyokuwa vitolewe kila kimoja kwa Tsh 300,000/= kwa watakaonunua vyeti hivyo.

Alisema jeshi la polisi lilifanikuwa kumkamata pia mmiliki wa steshenari hiyo Mgeni Nyabuzoki ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania pamoja na wafanyakazi wawili wa steshenari iliyokuwa ikitumika kutengeneza vyeti vyenye mihuri ya vyuo mbalimbali.

Watuhumiwa wote watano wanashikiliwa na jeshi la polisi watafikishwa mahakama pindi uchunguzi utakapokamilika lengo ikiwa ni kukomesha vitendo vya watu wanaoiibia serikali kwa kugushi nyaraka feki.


Akizungumzia tukio hilo, Mratibu wa maduka ya madawa ya Binadamu Muhimu kutoka Baraza la Famasia Taifa ,Dominic Mfoi alisema baada ya kuona kuna baadhi ya vyeti feki vinapelekwa ofisini kwao na baadhi ya watu wanaoomba ajira wakiwa hawana sifa wakapata wasiwasi na kuamua kufanya uchunguzi na kubaini zaidi ya vyeti 690 vinatengenezwa vinavyo weza kusababisha watu wasio na taaluma ya Afya kupatiwa ajira.


Alisema Wizara ya Afya na ustawi wa jamii jinsia wazee na watoto in autaratibu wake wa kutoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya Afya hivyo hali hiyo ya kugushi vyeti feki inaweza kusababisha wagonjwa kupatiwa sumu badala ya dawa kutokana na wahudumu wanaoajiriwa kukosa sifa na kutokuwa na ujuzi wowote kuhusiana na taaluma hiyo.

Mfoi alisema suala hilo la vyeti feki lina madhara makubwa kwa serikali na taifa kwa ujumla wanasubiri serikali itoe tamko kwa waliotumika kufanya uhalifu huo pia aliwaomba wamiliki wa maduka ya dawa kuwa makini katika kuwaajiri watu hivyo ni vyema wakaajiri watu wenye taaluma ya afya.

Na Rhoda Ezekiel- Malunde1 blog Kigoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post