Ofisi ya Rais -TAMISEMI inatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016.
Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na
wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na
Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740
sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka
2015 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo
mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya
tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu
ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya
www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI
Tumia link hii kupata matokeo :
==> Waliochaguliwa kidato cha tano awamu ya pili 2016
==>Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016
==> Waliochaguliwa kidato cha tano awamu ya pili 2016
==>Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016