Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha!! MKUU WA MKOA WA SHINYANGA NA VIONGOZI WENGINE WA MKOA WAKIFANYA USAFI HOSPITALI YA MKOA



Mkuu wa Moa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack ameongoza zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  wa Shinyanga pamoja na maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni kuendelea kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi.


Katika zoezi hilo lililoanza mapema saa 12 hadi saa 4 asubuhi, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, Viongozi wa Taasisi pamoja na Watumishi wa Sekta mbalimbali Mkoani hapa.
 Aidha, Mhe. Telack amezindua rasmi vifaa vya usafi vyenye thamani ya shlingi milioni sita vilivyotolewa na Taasisi ya "Americares"kwa ajili ya kuzolea taka pamoja na kubebea nguo za wagonjwa zinazohitaji kufanyiwa usafi.
Mhe. Telack ametoa wito kwa Wananchi wote kufanya usafi kwenye maeneo wanayoishi na wanayofanyia kazi kila wakati ili kujiepusha na maradhi yanayosababishwa na uchafu.Picha zote kwa hisani ya Magdalena Nkulu-Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga

Vifaa vya kufanyia usafi vilivyozinduliwa


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizindua vifaa vya kufanyia usafi, kulia ni Kaimu Mganga Mkuu  wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Mwita Ngutunyi, kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Bw. Albert Msovela na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Dkt. Daniel Maguja.



Usafi ukiendelea, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kushoto), Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mwita Ngutunyi kati kati na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakiwa wanafanya usafi katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Albert Msovela wakifanya usafi mbele ya jengo la Hospitali ya Mkoa


Usafi ukiendelea, Mkuu wa Mkoa kushoto, Katibu Tawala Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Shinyanga Muliro Jumanne Muliro



Mkuu wa Wilaya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro akiendelea na usafi

usafi unaendelea
Baadhi ya watumishi wakiendelea na usafi


Picha zote kwa hisani ya Magdalena Nkulu-Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com