Mfanyabiashara
Christon Mbalamula, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kulidhalilisha
Jeshi la Polisi kwa kudai anatangaza ndoa na askari watakaomhudumia
kama mume, huku akihoji kama wameshanunua mafuta ya kilainishi maarufu
KY JELLY.
Mshtakiwa
huyo alifikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana akikabiliwa
na shtaka la kutumia huduma ya mtandao wa kijamii wa ‘WhatsApp’
kulidhalilisha jeshi hilo.
Akisomewa
mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Dk. Yohana Yongolo, Wakili wa
Serikali, Winifrida Sumawe alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo
Agosti 26 mwaka huu katika eneo la Vijibweni Kigamboni.
Alidai
siku ya tukio, mshtakiwa alilidhalilisha Jeshi la Polisi baada ya
kutumia huduma ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp kusambaza ujumbe
unaosema. “Natangaza ndoa na askari yoyote atakayejipendekeza kwangu siku hiyo ataolewa bila mahari.
“Ataishi
kwangu bila nguo hadi operation Ukuta itakapoisha atapika na kupakua
na kunikidhi haja km mume wake, Note KY JELLY mmeishanunua so msiogope
nyie mapolice uchwara” alisema katika ujumbe huo.
Mshtakiwa huyo alikana shitaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.
Hakimu
Yongolo alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila
mmoja asaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni moja na mmoja kati ya
wadhamini hao awe na mali isiyohamishika yenye thamani isiyo chini ya Sh
milioni mbili. Mshtakiwa awe anaripoti kila baada ya wiki mbili kwa
msimamizi wa mawakili wa serikali.