News Alert!! BASI LA NEW FORCE LA DAR - SONGEA LAUA WATU 12,KUJERUHI 30 HUKO NJOMBE
Tuesday, September 20, 2016
Basi la New Force kutoka Dar es salaam kwenda Songea limepata ajali baada ya kupinduka eneo la Kifanya kilomita kadhaa kutoka mkoani Njombe. Ajali hiyo imetokea Septemba 19,2016 majira ya saa moja na dakika 40 usiku.
Inaelezwa kuwa watu 12 (wanawake 8,wanaume 4) wamepoteza maisha huku 30 wakijeruhiwa.
Abiria wa basi hilo wanasema basi lilikuwa katika mwendo kasi na kwamba lilinusurika kupinduka mara mbili na mara ya tatu ndipo likapinduka.
Social Plugin