Jeshi la polisi nchini limeondoa marufuku ya mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kwa madai kwamba limeridhishwa na hali ya kiusalama iliyopo nchini.
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani Mssanzya ametangaza kuondoa zuio hilo leo na kusema kuwa makatazo mengine ya mikutano ya vyama hivyo yako pale pale.
Mssanzya amesema mikutano ya hadhara na maandamano bado hairuhusiwi lakini wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao katika majimbo yao kwa mujibu wa katiba.
"Maandamano na mikutano ya hadhara imezuiliwa hadi tathmini pana zaidi ya hali ya usalama itakapofanyika," amesema Mssanzya
Social Plugin