YAH: KUKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII
Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha
taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba
kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina
ukweli wowote.
Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga
kuliweka Taifa kwenye taharuki. Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega
na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao
kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka
wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga
kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.
Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais
inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo
vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Social Plugin