Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTOTO AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNYWESHWA MITISHAMBA NA JIRANI YAKE DIDIA SHINYANGA



 
MTOTO Dominica Matenya (3) amefariki dunia kwa kudaiwa amenyweshwa dawa za miti shamba na jirani yake, Leah John katika Kitongoji cha Danduhu, Kijiji cha Didia kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mtendaji wa kijiji hicho, Waziri Shimba alisema tukio hilo lilitokea jana saa sita mchana ambapo alieleza kuwa alipata taarifa hiyo kutoka kwa majirani na kuanza kufuatilia.

Shimba alisema mtoto huyo alidaiwa kusumbuliwa na maradhi ya kuharisha na mwili kuwa na mabaka, ambapo jirani yao, Leah walikubaliana na mzazi wa mtoto kumpatia dawa za miti shamba, lengo likiwa ni kuondoa mabaka ya mwili. 

Diwani wa Viti Maalumu, Mengi Charles alisema walielezwa mtoto huyo aliamka akiwa hajazidiwa ila mwili wake ulikuwa na mabaka na ndio jirani yake akampatia dawa ya miti shamba ili kumwondolea mabaka ya mwili aliyokuwa nayo.

Mama wa mtoto, Thereza Omari, alisema kuwa mtoto wake alipoamka asubuhi alianza kuharisha kidogo huku akiwa na mabaka mwilini na jirani huyo alimueleza kuwa anayo dawa ya miti shamba itakayoweza kumtibu mabaka na akaamua kutompeleka hospitali.
Na Kareny Masasy-Habarileo Shinyanga
 
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com