MKAZI
wa Kijiji cha Kazibizyo Kata ya Ng’anzo, Wilayani Bukombe, Sebastian
Lumbe (36), amefariki dunia kisimani alimoingia kumuokoa mbuzi kwa
ujira wa Sh 6,000.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Misheni baada ya
mbuzi huyo kutumbukia kwenye kisima kinachodaiwa kuwa na urefu wa futi
30.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Misheni, Antony Kuya alithibitisha kutokea tukio hilo.
Alisema
baada ya mbuzi huyo kutumbukia kisimani, mmiliki wake, Marco Sylvester
alitangaza ujira wa Sh 6,000 kwa mtu ambaye angefanikiwa kumtoa na
ndipo Lumbe alipojitolea kuingia kisimani humo.
Alisema
kabla ya Lumbe kuingia kisimani humo na kukutwa na mauti, walijitokeza
watu wawili tofauti lakini kila walipoingia waligundua kisima hicho
kilikuwa kirefu.
Kwa sababu hiyo walighairi hadi alipofika yeye na kujitosa.
“Baada ya kuingia kisimani alianza kupiga kelele za kuomba msaada.
“Watu
waliokuwa karibu na kisima hicho walimtupia kamba lakini wakati
anajaribu kuivuta kupanda ilikatika na akaanguka kurudi kisimani.
“Baadaye
kijana mmoja, Leonard Mathayo aliingia kujaribu kumuokoa lakini wakati
akiwa humo ndani alisema baada ya kukaribia kufika mwisho wa shimo
alimkuta akitupa miguu.
“Alipoanza kumfunga kamba ili wamvute aliishiwa nguvu na kukosa hewa na hivyo ilimlazimu kuomba msaada kutoka nje,” alisema Kuya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo aliwaonya wananchi kuwa
waangalifu na visima virefu kama hivyo kwa sababu ni hatari.
Social Plugin