Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMME ALIYENAJISI WATOTO KANISANI AHUKUMIWA KIFUNGO JELA 100



MWANAMUME aliyenajisi watoto watatu kanisani,nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 100 jela baada ya Mahakama ya Kaunti ya Embu nchini Kenya kumkuta na hatia ya kutenda unyama huo.

Mtuhumiwa huyo, Harrison Kinyua, alihukumiwa kifungo hicho na Hakimu Maxwell Gicheru baada ya kuridhika na ushahidi kuwa aliwanajisi wanafunzi wawili wa kike wenye umri wa miaka 13 na 10.

Kinyua alitenda unyama huo Desemba 10, mwaka jana katika kanisa hilo lililopo Kijiji cha Kangaru, Kaunti ya Embu.

Wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo, mahakama iliambiwa Kinyua aliwanajisi wanafunzi hao walipokuwa wakirudisha viti walivyokuwa wamechukua kanisani humo.

Alifunga mlango wa kanisa hilo na kisha akawaagiza kulala chini kabla ya kuwanajisi.

Upande wa mashtaka ulisema Kinyua alimfukuza msichana wa tatu aliyekuwa ameandamana na waathirika akidai hakuwa na matiti.

Baadaye aliwapa waathirika Sh 20 (za Kenya) kila mmoja na kuwataka waende kununua chips katika soko la karibu. Lakini wazazi wao waligundua hilo na kuripoti kwa polisi.

Dk. Christine Nyangilo wa Hospitali ya Embu Level Five, aliiambia mahakama kuwa vipimo vilithibitisha wasichana hao wa umri wa miaka 13 na 10 walinajisiwa.

Alisema waathiriwa walipelekwa hospitalini Desemba 10 huku nguo zao zikiwa zimechafuka.

Awali Kinyua alikanusha mashtaka hayo akisema kuwa masaibu yake yalitokana na uhasama uliopo baina yake na familia za waathiriwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com