RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za Sikukuu ya Eid-El-Adh-ha maarufu kama ‘Eid ya Kuchinja’ itakayofanyika Septemba 12, mwaka huu (Jumatatu ijayo).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waisalam Tanzania (BAKWATA), Salim Abeid amesema kuwa sikukuu hiyo kitaifa itafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya BAKWATA kuanzia saa 1:30 asubuhi huku akiwataka waumini wa dini ya Kiislam kujitokeza kwa wingi.
Katika waraka wake kwa waandishi wa habari, Abeid aliongeza kuwa, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuber bin Ally anawatakia Waislam wote na wananchi kwa jumla sikukuu njema Sikukuu ya Eid-El-Adh-ha.
Social Plugin