Bongo Movie Shinyanga inakuletea filamu ya kusisimua,kutisha,kuhuzunisha,kufurahisha,kuonya na kuelimisha inaitwa “Nyama ya Ulimi”.
Nyama ya Ulimi ni filamu matata yenye kiwango cha kimataifa kutoka kwa waigizaji waliobobea katika sanaa ya uigizaji mkoani Shinyanga na itazinduliwa hivi karibuni kwani kila kitu kimekamilika,angalia hapo chini nimeamua kukuonjesha walau kwa picha 8 na video fupi kukuweka mkao wa kula kupokea kazi nzuri ya wasanii kutoka Shinyanga.
Filamu hii ya kiafrika pamoja na mambo mengine inazungumzia kwa kina masuala ya ukatili wa kijinsia/manyanyaso wanayofanyiwa wanawake katika ndoa na jamii kwa ujumla.
Filamu hii inamfanya binadamu yeyote katili kwa wanawake awe na adabu kwa wanawake wote duniani lakini pia inamfanya mwanamme asiyejielewa apate akili timamu kabla ya kujutia kauli zake chafu kwa wanawake.
Mwongozaji mkuu/Director wa Filamu hii ,David Skela ameiambia Malunde1 blog leo Ijumaa,Septemba 30,2016 kuwa Filamu ya “Nyama ya Ulimi” yenye scene 20 imechezwa na wasanii kutoka Shinyanga.
“Project inaonesha mkoa wa Shinyanga na Tabora,ujumbe unafikia dunia nzima,wahusika wakuu wapo wanne ambao ni Songoro Gaddafi “Songoro”,Charles Sunday,Mariam Billal “Mercy” na Siha Mtui “Siha”,tunaomba watanzania na wapenzi wa filamu duniani kote waipokee filamu hii,ambayo inaonesha kiasi gani wanaume wenye pesa na wasio na pesa wanavyonyanyasa wanawake katika ndoa zao”,amesema Skela.
Akizungumza na Malunde1 blog ,mwenyekiti wa Bongo Movie mkoa wa Shinyanga bwana Juma Ibrahim Songoro amesema filamu hiyo iko tayari na itazinduliwa rasmi hivi karibuni wanachofanya sasa ni kutafuta wadhamini wa filamu yao ya “Nyama ya Ulimi” ambayo wanaamini itafikisha ujumbe dunia nzima kuwa sasa ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake sasa unatosha.
"Kauli mbiu tuliyotumia katika Filamu hii,ambayo itazinduliwa muda wowote kuanzia sasa ni "Kwa pamoja tunaweza kutokomeza Unyanyasaji kwa wanawake",tunaamini itapokelewa siyo tu kitaifa bali ni kimataifa",amesema Songoro.
Ninazo hapa baadhi ya picha na video fupi ikionesha walau kidogo mambo mazito yaliyomo katika Filamu/Movie ya “Nyama ya Ulimi”
Zaidi wasiliana na Songoro kwa simu namba 0767831036
Songoro Gaddafi

Mercy
Nimeamua kukuonjesha kidogo...Naomba utumie dakika zako mbili tu kutazama "Filamu ya Nyama ya Ulimi"
Bonyeza hapa chini
Zaidi kuhusu "Filamu ya Nyama ya Ulimi"wasiliana na mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga Juma Ibrahim Songoro kwa simu namba 0767831036
Social Plugin