Benki ya NMB Manonga mjini Shinyanga imenusurika kuungua moto baada ya jengo lililopo jirani na benki hiyo mali ya bwana Mohammed kuteketea kwa moto.
Jengo lililoteketea kwa moto lipo katika mtaa wa Miti Mirefu karibu na Benki ya NMB Manonga na sheli ya mafuta mjini Shinyanga.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa moto huo uliibuka jana Septemba 20,2016 majira ya saa moja jioni huku chanzo kikielezwa kuwa ni mtungi wa gesi ulikuwa jikoni.
Hata hivyo Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga likishirikiana na wadau mbalimbali lilifanikiwa kuzima moto huo majira ya saa tatu na nusu usiku na kufanikiwa kuokoa mali zilizokuwa katika robo tatu ya jengo hilo lililopo karibu na sheli ya mafuta pamoja na kuzuia madhara yasitokee kwenye benki ya NMB.
Inaelezwa kuwa robo ya jengo hilo imeungua na vitu vilivyokuwemo navyo vimeungua katika robo ya jengo hilo na kwamba hakuna majeruhi na hasara iliyopatikana bado haijajulikana
Moto ukiwaka karibu na benki ya NMB Manonga(kushoto)
Zoezi la kuzima moto likiendelea |
Social Plugin