Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: THRDC YAWAPIGA MSASA WAHARIRI,WAANDISHI NA VIONGOZI WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba nchini, Amon Mpanju akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,Wahariri,Viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini na taasisi mbalimbali wakati wa siku ya utoaji wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Seashells jijini Dar es salaam leo Septemba 28,2016.
 
Warsha hiyo imelenga kufanya tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini ikiwa ni sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa haki za binadamu.Pamoja na mambo mengine Mpanju alisema serikali haiungi mkono ndoa za jinsia moja na kuwataka wadau kuungana kupiga vita ndoa hizo ambazo kwa mujibu wa sheria na tamaduni za kitanzania hazikubaliki.Picha zote na Kadama Malunde wa Malunde1 blog na Geofrey Adroph wa Pamoja blog



Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition- THRDC) Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza jambo kwa waandishi wa habari pamoja na viongozi wa klabu za waandishiwa habari (press clubs) wa mikoa mbalimbali waliokutana kujadili changamoto wanazozipata pamoja na kujadili rasmu ya sheria mpya itakayopitishwa bungeni hivi karibuni.


Rais mstaafu wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akiwaomba viongozi wa press club waliofika katika mkutano uliokuwa ukijadili mswada wa sheria mpya ya vyombo vya habari







Baadhi ya viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini pamoja na wadau mbalimbali wa habari wakiendelea kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
 
ENDELEA KUANGALIA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Warsha inaendelea


Wenyeviti wa Press Clubs mbalimbali katika pozi


Wenyeviti wa press clubs wakibadilishana mawazo



Washiriki katika picha ya pamoja




Picha za kumbukumbu














Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com