Kiongozi
huyo wa Chadema na wafuasi hao 18 walikuwa wakishikiliwa katika
mahabusu za jeshi la polisi kwa tuhuma za kuandaa na kuhamasisha
maandamano na mikutano ya Oparesheni ya chama hicho iliyopewa jina la
UKUTA, ambayo ilipigwa marufuku na jeshi hilo.
Walifanikiwa
kupata dhamana baada ya Hakimu wa Mahakama hiyo kueleza kuwa ameridhia
hoja za upande wa utetezi baada ya kusikiliza pande zote mbili na
kubaini mapungufu kwenye maombi ya upande wa mashtaka.
Awali,
Mwendesha mashtaka aliitaka Mahakama hiyo kuwanyima dhamana washtakiwa
hao kwa madai kuwa endapo wataachiwa wataendelea kufanya kosa hilo.
Hata
hivyo, Hakimu alitupilia mbali maombi hayo akieleza kuwa wameshindwa
kuthibitisha pasipo shaka kuwa endapo washtakiwa hao wataachiwa
watafanya tena kosa hilo.
Pia,
Hakimu alieleza kukubaliana na hoja ya washtakiwa hao kuwa hati ya
kiapo iliyowasilishwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka ilikuwa na
mapungufu ya kisheria.
“Ninakubaliana na upande wa utetezi kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa ina mapungufu ya kisheria,” alisema Hakimu baada kupitia na kugundua kuwa aliyesaini hati hiyo sio anayeonekana kuitoa.
Washtakiwa
wote walitimiza masharti ya dhamana kwa kuwasilisha wadhamini wawili
kila mmoja ambaye ataweka dhamana ya shilingi milioni 3.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria
mahakamani hapo na kuondoka na Salum na wafuasi hao ambao walifikishwa
mahakamani hapo awali chini ya ulinzi mkali. Kesi imeahirishwa hadi
Oktoba 4 mwaka huu
Social Plugin