*****
Watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kupata mshtukio baada ya kupigwa na radi wakiwa wamejikinga na mvua kwenye mti katika kijiji cha Tundu kata ya Busangi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea jana Septemba 17.09.2016 saa 2:30 mchana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Fikiri Paskali (35) na Maneno Luzalia (16) wakazi wa kata hiyo na watano waliopata mshtuko katika tukio hilo walipata matibabu katika zahanati ya Busangi na hali zao ni nzuri..
Social Plugin