Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa
kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi
kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu
makundi yafuatayo kuomba udahili.
- Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
- Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
- Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
- Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,
- Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
- Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili
kuruhusu taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya
Mikopo na vyuoni.
Asanteni
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
02 Septemba 2016
Social Plugin