Utaratibu wa Malunde1 blog kila weekend ni kukusogezea nyimbo za asili...Leo tunakukutanisha na Msanii machachari wa kike anayeimba kwa lugha ya Kisukuma..anaitwa "Sengi Milembe" kutoka mkoani Simiyu lakini sasa anaishi Buhongwa jijini Mwanza.
Mwanamama huyu ametualika kutazama video yake inaitwa "Nesi" iliyotengenezwa katika studio za Bicon zilizopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Katika wimbo huu unaoitwa Nesi ,Msanii Sengi "Shangazi" Milembe amezungumzia visa vya nesi aliyeamua kuoana na mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodini.
Itazame hapa ngoma hii kali,wanenguaji nao balaa kweli kweli...utafikiri hawana mifupa.
Itazame hapa ngoma hii kali,wanenguaji nao balaa kweli kweli...utafikiri hawana mifupa.
Social Plugin