Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA YASHINDWA KUTOBOA REKODI YAO DHIDI YA NDANDA FC NANGWANDA



Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Septemba 7,2016 kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja vya Taifa Dar es Salaam, Sokoine Mbeya na uwanja wa Nangwanda Sijaona Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans walisafiri wakitokea Dar es Salaam kwenda Mtwara kuwafuata Ndanda FC kwao.



Hata hivyo Yanga ambao walikuwa wanatarajiwa kukutana na upinzania mkubwa kutoka kwa Ndanda FC kutokana na rekodi ya mechi zao za nyuma, Yanga wamelazimishwa suluhu ya 0-0 baada ya Ndanda kufanikiwa kucheza mchezo wakulinda goli lao kwani kipindi cha pili walicheza nyuma zaidi.



Huu ni mchezo wa tano kwa Yanga na Ndanda FC kukutana katika Ligi Kuu soka Tanzania bara, lakini ni mara ya pili kwa timu hizo kucheza katika uwanja wa Nangwanda huku Yanga akiwa kafungwa mara moja katika uwanja huo na kutoa suluhu mara moja, kwa ujumla Yanga na Ndanda wamefungana mara moja moja na kutoka sare mara tatu.



Matokeo ya mechi nyingine za VPL zilizochezwa leo September 7
Simba SC 2-1 Ruvu Shooting
Tanzania Prisons 0-1 Azam FC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com