Chama
cha ACT-Wazalendo kimesema kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya kiongozi
wake wa chama, Zitto Kabwe kwamba ana miliki mali za kifisadi pamoja na
kuhusishwa na ununuzi wa ardhi maeneo ya Kigamboni uliofanywa na NSSF
kwa bei ya milioni 800 kwa ekari moja, wakati bei halisi ni milioni 25
na kwamba kitendo hicho kimeitia hasara serikali .
Tuhuma
hizo zilitolewa jana na Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Christopher Ole Sendeka, ambapo alivitaka vyombo vya uchunguzi kufanya
uchunguzi katika shirika hilo ili kubaini waliohusika kwa ajili ya
kuchukuliwa hatua za kisheria, huku akimhusisha Zitto katika uchunguzi
huo.
Ole
Sendeka alitaka akaunti za benki za Zitto pamoja na maisha yake binafsi
kuchunguzwa kama yana uhalisia na kipato chake halali.
Tuhuma
hizo zimekiibua chama cha ACT, ambapo leo Katibu wa Bunge na Serikali
za Mitaa ACT, Habibu Mchange amevitaka vyombo vya uchunguzi haraka
iwezekanavyo kuchunguza mali, madeni, akaunti zote za benki pamoja na
mfumo wa maisha ya Zitto.
“ACT
imeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa
jana na Ole sendeka dhidi ya kiongozi wa chama chetu,” amesema.
Amesema
kuwa, katiba ya chama hicho huwataka viongozi wote kuweka hadharani
matamko ya mali zao na madeni na kwamba Zitto alitekeleza matakwa hayo
ya kisheria hivyo mali na madeni yake yako hadharani na mtandaoni.
“Tunaamini kama kuna kiongozi ambaye mali, madeni, maslahi, na akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto,” amesema.
Aidha,
Mchange amedai kuwa, kilichomsukuma Sendeka kutoa tuhuma hizo kwa Zitto
ni harakati zake za kuupinga muswada mpya wa habari.
“Tuhuma
za ole sendeka kuna kitu nyuma yake, jitihada za zito za kupambana na
mswada wa habari ndizo zilizomuibua, sababu wanataka upitishwe ili
kuviua vyombo vya habari,” amesema.
Amesema ACT itaendelea kuisimamia serikali katika mambo ya bungeni kama anavyofanya mbunge na kiongozi wao wa chama.
Social Plugin