Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA BAADA YA KUMLAWITI MWANAMME ALIYEMFUMANIA AKIHONDOMOLA TENDO LA NDOA NA MKE WAKE


Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha jela, Erick Kasila (39) baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka matatu likiwamo la kumlawiti mwanamume kwa madai kuwa alimfumania gesti na akiwa na mke wake.


Kasila anadaiwa kumlawiti (Mwanamme mwenzake jina tunalo) katika nyumba ya kulala Wageni ya Maembe, Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala na kumpiga picha za utupu na kutishia kutuma katika mitandao ya kijamii na kumnyang’anya nguo alizovaa, fedha, laptop na viatu.


Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Juma Richard (31) alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mlalamikaji kumnyonya uume wake na kumtaka kusaini karatasi ya ahadi ya Sh1 milioni ili asisambaze picha walizompiga wakati wakimlawiti, ambazo hata hivyo, walizisambaza katika mitandao ya kijamii.


Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said Mkasiwa alisema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano dhidi ya washtakiwa na vielelezo vya picha zinazoonyesha mlalamikaji alikuwa analawitiwa, nyingine zikionyesha mshtakiwa akimlazimisha mlalamikaji amnyonye sehemu zake za siri.


Akipitia baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Mkasiwa alisema kulawitiwa kwa mwanamume huyo ni baada ya kukutwa na (mwanamke jina tunalo) ambaye ni mke wa Kasila.


Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa hao kwa kitendo walichokifanya ambacho kimemuathiri mlalamikaji kisaikolojia.


Washtakiwa walipopewa nafasi ya kujitetea kwa nini wasipewe adhabu kali, walishindwa na badala yake waliomba nakala ya hukumu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com