Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI:
AJALI YA
GARI LA POLISI KUACHA NJIA / KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI.
TAREHE 05/10/2016 MAJIRA YA 09:50 KATIKA KIJIJI CHA SHILABELA, KATA YA
PANDAKICHIZA, TARAFA YA NINDO, WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI MKOA WA SHINYANGA GARI NAMBA PT. 1886 TOYOTA
LAND CRUISER MALI YA MKUU WA POLISI WILAYA YA SHINYANGA LIKIENDESHWA NA DEREVA
WA POLISI LIKIWA KWENYE SHUGHULI ZA MWENGE WA UHURU LILIACHA NJIA NA KUGONGA
GEMA UPANDE WA KULIA MWA BARABARA , KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA
ASKARI:
(1)PF. 18763
INSP ZITTA AMBAYE AMEUMIA MKONO WA KULIA
(2)WP.10550
PC MARIAM AMBAYE AMEUMIA KIUNO
(3)H.6012 D/C YENYE AMBAYE AMEUMIA KIFUA NA
GOTI LA MGUU WA KULIA
(4)G.1660 PC PAULO AMBAYE AMEUMIA KICHWANI
(5)G.7091 PC JOHN AMEUMIA GOTI MGUU MGUU WA
KUSHOTO NA MCHUBUKO KATIKA VIDOLE VYA MKONO WA KULIA
(6)H.4740 PC FREDY - AMEUMIA BEGA LA KULIA NA
MICHUBUKO MKONO WA KUSHOTO (7)G.4381 PC MOHAMED - AMEUMIA MAKALIO MGUU WA KULIA
(8)H.5937
D/C JOSEPHAT - AMEUMIA GOTI LA MGUU WA KULIA NA
(9)J.1101 PC ALBANO - AMEUMIA BEGA LA KUSHOTO .
HALI ZA MAJERUHI ZINAENDELEA VIZURI AMBAPO
WAMEPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA NA KURUHUSIWA KWANI
HALIZAO NI NZURI KASORO ASKARI WATATU
AMBAO BADO WANAFANYIWA UCHUNGUZI
ZAIDI LAKINI HALI ZAO SI MBAYA.
KIINI CHA
AJALI HIYO NI BARABARA AMBAYO SI NZURI.
UHARIBIFU WA GARI PIA SI MKUBWA.
IMETOLEWA NA
MULIRO J MULIRO (ACP) RPC SHINYANGA.
Social Plugin