Baada
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia msemaji wake Christopher Ole
Sendeka kusema kuwa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Edward Lowassa, kuwa si tishio kwa CCM.
Jumamosi
ya Oktoba, 29 Chadema imejibu kuwa Lowassa pamoja na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA) utaendelea kuwa tishio kwa chama hicho na kwamba CCM
ijiandae kuachia madaraka mwaka 2020 kwa kuwa imejipanga kuchukua dola.
Mkuu
wa Idara ya Uenezi Chadema Taifa, Hemed Ali wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es
Salaam amesema Lowassa ni tishio kwa kuwa alipokihama chama hicho
aliacha mpasuko na kudai kuwa aliondoka na nguvu ya chama hicho.
“CCM
wana homa kubwa iitwayo Lowassaphobia na ndio maana imeacha kuendelea
na shughuli zao na kumuandama Mjumbe wa kamati kuu wa chama chetu
Lowassa. Kimsingi mchakato wa kumpata Mgombea Urais na Mgombea mwenza wa
chama chetu ulikuwa wa kidemokrasia kwa mujibu wa katiba yetu ambapo
ibara (7.7.16 (a) kamati kuu inapewa mamlaka ya kuwafanyia utafiti
wagombea Urais wa chama chetu na kupeleka ripoti Baraza kuu,
“Baraza
kuu la chama kwa mujibu wa katiba ( 7.7. 13 (a)) inapendekeza majina ya
wagombea au mgombea aliejitokeza na hatimae kwa mujibu wa katiba
(7.7.10 (c)) Mkutano mkuu wa chama utachagua mgombea Urais na Mgombea
Mwenza,” amesema na kuongeza.
”
Lowassa alipitia hatua zote kama mwanachama halali wa CHADEMA mwenye
haki sawa na mwanachama yeyote kwa mujibu wa katiba (5.1) na (5.2)
kimatendo na kiimani kwa kufuata katiba , nilitaraji Sendeka aeleze kile
kiini macho cha kumchagua Ndugu Magufuli Dodoma kuwa Mgombea wao huku
wenyewe kwa wenyewe wakipinga mchakato wa kumpata usiofuata katiba na
kanuni za chama hicho kama walivyojitenga na uamuzi huo baadhi ya
wajumbe wa kamati kuu ile kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa
maamuzi ndani ya vikao.”
Amedai
kuwa, Kamati Kuu yao ilipasuka katikati baina ya wajumbe wake na kudai
kuwa wajumbe waliokuwa wanamuunga mkono Lowassa, wengi wao
hawakuchaguliwa kushika nyadhifa serikalini .
“Ni
kawaida ya CCM kuchafua mtu ambae atakua na msimamo na nia ya kulivusha
taifa , Wamefanya hivyo kwa viongozi wetu wa chama na watu binafsi
hivyo hatushangai walivyo mshambulia Lowassa akiwa ndani ya CCM na hata
Sasa CHADEMA. Sendeka amesema kuwa yupo kiongozi ndani ya chama chetu
aliyepata dola milioni 15 takribani bilioni 33 eti apangesafu ya uongozi
ndani ya chama,
“Kiuhalisia
na kwa hesabu ndogo tu ni kuwa pesa hiyo si tuu kuwa inatosha kwa ajili
ya kupanga uongozi ndani ya chama bali ni inatosha kwa ushindi wa
mitaa, kata na halmashauri , ubunge na urais hivyo wakati anataja
tarakimu hizo ajue na michanganuo ya kimahesabu badala ya kuwa
mkurupukaji na ningemuelewa kama angekuja hadharani kuaga rasmi kwa
niaba ya chama chake na kutupisha kuwatumikia watanzania kuliko kuongea
uongo,” amesema.
Social Plugin