Idadi
ya wanafunzi ambao tayari wamepitishwa kupata mkopo ni 7,904, hata hiyo
imeelezwa kiwango hicho kitaendelea kubadilika kwa kuwa mchakato
unaendelea.
Taarifa
iliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Stella Manyanya ilibainisha kuwa bodi imekamilisha uchambuzi wa majina
ya waombaji ambao wana sifa zinazotakiwa na majina ya wanufaika wapya
ambayo yameanza kutangazwa kupitia tovuti ya bodi hiyo.
“Kwa
kuzingatia mpango mkakati, pia mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka
2016/17, Serikali imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji
mikopo,” alisema Manyanya.
Alitaja
vigezo vilivyotumika kuwa ni pamoja na vipaumbele vya kitaifa
vinayoendana na mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano, Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu
wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele.
Manyanya
alizitaja fani zilizopewa vipaumbele kuwa ni sayansi za tiba na afya,
ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo,
mafuta na gesi asilia, sayansi asilia na mabadiliko ya tabianchi,
sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.
Katika
taarifa yake, Manyanya alisema pia mchakato wa kuwapata wenye sifa za
kukopa uliangalia uhitaji wa waombaji, hususan wenye mahitaji maalumu
kama walemavu na yatima, ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele
na umahiri.
“Kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao katika vipengele vyote vya mikopo,” alisema.
“Kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao katika vipengele vyote vya mikopo,” alisema.
Akizungumzia
mchakato huo, mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo, Abdul Badru alisema
unaendelea kufanywa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na timu ya bodi
imejigawa katika vikundi ili kuhakikisha mipango inakwenda jinsi
inavyotakiwa.
“Timu
ipo kazini na inafanya kazi yake kwa umakini. Kwa sasa majina ya
waliochaguliwa kutokana na vigezo yamewekwa, lakini ni wahusika wenyewe
au walezi na wazazi ndiyo wanaweza kuyaona kupitia namba zao za usajili
wa kidato cha nne. Lakini siku chache zijazo tunaweza kuwataja
wakaonekana kwa kila anayehitaji kuyaona,” alisema Badru.
Social Plugin