Ikiwa imepita siku mbili tangu aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa
tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mwamvuli wa
UKAWA, Edward Lowassa kueleza tathmini ya utendaji kazi wa serikali ya
awamu ya tano chini Rais John Magufuli, ambapo alidai kuwa, katika
kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi huo, kumekuwepo na ukiukwaji wa
misingi ya demokrasia na utumishi wa umma kuwa kaa la moto.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimevunja ukimya na kumjibu kwa kusema kuwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita alikuwa wa kwanza kukiuka misingi ya demokrasia. Kuhusu utumishi wa umma kuwa kaa la moto, imemjibu kuwa wanao lalamika hivyo ni wale wanaotumiwa kuficha mafisadi na wakwepa kodi.
Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka amewaambia waandishi wa habari kuwa Lowassa hastahili kuituhumu serikali ya Rais Magufuli kuwa inakiuka misingi ya demokrasia.
“Demokrasia ya kweli lazima ianze ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea kuvigharamia kwa kuamua kumteua mgombea mtunguo ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania?,” amehoji.
Ole Sendeka ameongeza kuwa “Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kulidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia.”
Amesema CCM haigopeshwi na matamko ya Lowassa anayotoa katika vyombo vya habari kwa kuwa havitaiathiri na kwamba imemamua kumjibu kwa madai kuwa anapotosha umma kwa kueleza mambo yasiyo na ukweli.
Ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko.
“Wanasayansi wa masuala ya siasa waiangalie demokrasia ya CHADEMA na UKAWA inavyofanya kazi maana ni kihoja, watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge viti maalumu. Kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA,” amesema.
Pia Sendeka amemtaka kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo kutoichukia serikali ya Rais Magufuli kwa kuwa inatekeleza yale aliyokuwa anayapigania.
“Chuki ya Zitto ya kuendelea kunyooshea kidole serikali ya CCM haina tija, sababu inatekeleza yote aliyokuwa akiyapigania,” amesema.
Katika hatua nyingine, Sendeka amedai kuwa CCM haijashiriki kukihujumu chama cha Wananchi (CUF) kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa kuwa kinawachonganisha viongozi wa chama hicho ili kigawanyike.
“Hatuna haja ya kuhangaika na CUF na wapanga siasa za uongozi CHADEMA, hatujashiriki kukivuruga na hatuna muda huo,” amesema.
=======

Ndugu wanahabari,
Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taarifa za upotoshaji
zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo
vya habari zinazolenga kukejeri, kudhihaki, kukatisha tama, kubeza na
kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Seikali zake
katika kuleta maendeleo kwa Watanzania
Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo
hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika
habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania
Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala
mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na
kuichafua taswira ya nchi yetu.
Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na
kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa
maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua
nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni
watanzania. Je ni tama ya madaraka tu au mengine?. Hakuna anayepinga
ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema
Ndugu wanahabari,
Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa
tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward
Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita tathimini ya
mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa octoba 25,2015
Katika taairifa yake, alidai kuwa alileta msisimko mpya katika siasa za
Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi yetu maana ya
demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais.
Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki na kuheshimu mawazo
ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii, tunajiuliza
ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa nayo?
- Tulishuhudia akiwa mgombea Urais wa chama ambacho hakijui, hakushiriki
kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya kupeperusha
bendela huku katiba na kanuni ya chama hicho ikivunjwa. Kidemokrasia
anayepewa fursa ya kupeperusha bendela ya chama chochote makini duniani
ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo,
kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi
ya chamahicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi
dhamira ya chama husika machoni kwa wananchi.
- Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama, ni demokrasia ipi
inayotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao
haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi,
kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua mgombea “MTUNGUO”
(ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo hicho cha
kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua
na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya
demokrasia
- CHADEMA watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu.
Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya viongozi kuteua
wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi aliteua
maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu
wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM.
Msingi wa kawaida wa kupata wabunge wa viti maalumu ukiacha kura za
maoni, kigezo kingine muhimu ni mchango wa mgombea / mwanachamahuyo
katika kukijenga na kukitumikia chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA
kwenye wabunge wake wa viti maalumu ni mapya kwenye ulimwengu wa
demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa kufanya utafiti wa
aina hii mpya ya demokrasia
Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa wangelikuwa
wamejifanyia tathimini, kujikosoa, kujisahihisha, na hata kufanya
uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi
ya demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao
Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutokuchukulia kwa wepesi
masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo za kuburudisha au
kutoa matumaini hewaq kwa wanachama na wananchi. Kanuni mojawapo ya
demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na
katika utekelezaji wa muundo huo
Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuuza sera ili
kujenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya wananchi.
Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia demokrasia itakavyoendeshwa
katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa mmoja wa
vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia
kupanga safu yake ya uongozi
Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano ya mara kwa mara ya
baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za nchi kuja Dar
es Salaaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha
viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kafanikisha mpango huo.
Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli, ameendelea kufanya juhudi kubwa
katika kujenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya utumishi
serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha,
kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na
wajibu kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa
umma kaa la moto.
Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa
miundombinu ya barabara, reli, afya na kununua vitanda vya wazazi, kutoa
elimu burekuanzia shule ya msingi mpaka sekondari na nyinginezo
hazipaswi kukatishwa tama kwa maslahi ya wachache ni vyema kuziunga
mkono kwa maslahi ya taifa letu
Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk. Magufuli madarakani, CCM
inawaomba wananchi kuendelea kummunga mkono katika dhamira yake safi
yakuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea maendeleo ya
kiuchumi na kijamii.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na;-
CHRISTOPHER OLE SENDEKA
MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM
28/10/2016