Meya
wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi amefikwa na
umauti jana majira ya saa tatu na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.
Taarifa
za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake, Dk. Makongoro Mahanga
ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za msiba huo
na kwamba leo watatoa taarifa rasmi na taratibu nyingine.
“Taarifa
za kifo cha Dk. Masaburi ni za kweli ingawa sijaenda hospitali,
ninafanya mawasiliano na familia lakini taarifa kamili kuhusu msiba
zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye tutamteua usiku huu, na
kesho (leo) tutaeleza kiundani,” Alisema Dk. Mahanga jana usiku.
Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Mtandao
huu unatoa pole kwa Taifa kwa ujumla kwa msiba huu wa aliyekuwa
kiongozi wa ngazi mbalimbali akiutumikia umma. Apumzike kwa Amani.
Amina!
Social Plugin