Kauli
hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na
wanachama wa chama hicho katika kikao cha ndani, kilichofanyika Wilaya
ya Kinondoni ambapo alisema Chadema kushindwa kutekeleza Operesheni
Ukuta ni dhahiri chama hicho kimeshindwa kutekeleza kile wanachoahidi
kwa Watanzania.
Alisema
mpaka sasa kumekua na vikao mbalimbali vinavyofanywa na viongozi wa
Chadema kwa ajili ya kuivuruga CUF, jambo ambalo alisema haliwekezani.
“Chadema
wanajitahidi kutuvuruga kwa kutuma waasi wa chama hiki, lakini naomba
niwaambie hawawezi, CUF ni ngangari hata serikali inajua na
wanachokifanya ni kupoteza muda bure.
“Unajenga Ukuta wa biskuti, ukiumwagia juisi unamong’onyoka, Ukuta gani huo, huu muziki wa CUF ni ngangari hawauwezi,” alisema Lipumba.
Alisema
katika kipindi hiki ambacho wana kesi mahakamani, wanachama wa chama
hicho wataendelea na shughuli za kukijenga chama hicho pamoja na
kuwasisitiza kuwa na msimamo wa kutetea chama na katiba yake, jambo
ambalo linaweza kuwasaidia kufikia malengo waliyokusudia ya kushika dola
kafika Uchaguzi wa mwaka 2020.
Alisema
kutokana na hali hiyo, rasilimali za chama hicho zinasimamiwa kwa
umakini chini ya walinzi wa chama hicho, Blue Guard ambao Katibu Mkuu wa
chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema ni wavamizi hawatambui.
“Ninamshangaa
Maalim Seif sasa hivi anaibuka na kusema hawatambui walinzi wa chama
Blue Guard ambao miaka yote walikua wanamlinda pamoja na rasilimali za
chama, lakini hayo yamekwisha nitazidi kumwomba aje tujenge chama hata
kama kesi inaendelea mahakamani,” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano anayemunga mkono
Profesa Lipumba, Abdallah Kambaya alisema kupoteza nafasi ya umeya na
naibu wake katika Manispaa ya Kinondoni ni matokeo ya mgogoro wa CUF na
kutokuwepo ushirikiano ndani ya Ukawa.
“Maalim
Seif anaunga mkono Ukawa, mbona wanachama wa Ukawa wameshindwa
kutusaidia ili kupata meya na naibu wake kwenye uchaguzi wa leo?
(jana),” alihoji.