Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKUU WA SHULE ASHUSHWA CHEO KWA KUWAKATAZA WANAFUNZI KUVAA SARE ZA MAGUFULI


Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kasamwa ya mkoani Geita, Dennis Otieno anadaiwa kushushwa cheo kutokana na kuzuia wanafunzi kuvaa sare za CCM kwenye mahafali ya kidato cha nne.


Pia, taarifa hizo zinasema mkuu huyo wa shule alipinga kitendo cha baadhi ya walimu kuchangisha fedha wazazi wa watoto ambao ni wanachama wa Klabu ya Magufuli ili kufanya sherehe hilo kutokana na agizo la Rais la kufuta michango yote mashuleni.


Otieno, ambaye alikataa kuzungumzia suala hilo, anadaiwa kushushwa cheo kutokana na shinikizo la makada wa chama hicho tawala, hasa mwenyekiti wa CCM mkoani Geita, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, ambaye amethibitisha kushushwa cheo kwa mtumishi huyo wa umma.


Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinasema Otieno aligombana na mwalimu ambaye ni mlezi wa Klabu ya Magufuli kutokana na kuandaa mahafali hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com