Mahakama
ya Mwanzo Iringa Mjini imemuachia huru mwalimu wa Shule ya Sekondari
ya Kiwele baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani katika kesi ya
kumtukana mwanafunzi.
Mwalimu
huyo, Elizabeth Maliga (32) ameshtakiwa kwa madai ya kumtukana
mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, Rehema Mwakatobe na mama yake.
Amedaiwa
kufanya kosa hilo wakati akimsainia Rehema barua ya kumuita mama yake
kwenda shuleni hapo kusikiliza kosa la kuchelewa shuleni.
Hukumu
hiyo imetolewa wakati Taifa likiwa kwenye mjadala mkubwa baada ya picha
za video zilizosambaa mitandaoni kuonyesha kundi la walimu wa Shule ya
Sekondari ya Kutwa ya Mbeya likimshambulia mwanafunzi Sestian Chikungu.
Tayari
Serikali imeshatangaza kuwafukuza chuo walimu hao na Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.
Akisoma
hukumu ya kesi hiyo iliyochukua takriban dakika 45, Hakimu wa Mahakama
hiyo, Abdallah Kutvai alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuishawishi
mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.
“Jukumu
la kuthibitisha kosa ni la upande wa mashtaka. Hiyo ni kwa mujibu wa
kifungu cha tano cha Sheria ya Ushahidi ya Mahakama ya Mwanzo
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
“Mashahidi
wa upande wa mashtaka wametofuatiana tarehe za kutendwa kosa hilo.
Shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji anasema kosa limetendeka
Septemba 13, mwaka huu kwenye kikao cha kujadili mwenendo wa utekelezaji
wa adhabu zilizotolewa na walimu kwa wanafunzi shuleni hapo,”alisema Hakimu Kutvai.
Amefafanua
kuwa shahidi namba mbili alishindwa kubainisha siku ya tukio na kutaja
tarehe tatu tofauti, ambazo ni Septemba 13, 14 na 15, siku ambayo
mwanafunzi huyo alipewa barua ya kurudishwa nyumbani kwao Dar es Salaam
kumfuata mzazi.
Social Plugin