Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
****
Hapa ni katika ukumbi wa mikutano katika Hotel ya Liga mjini Shinyanga ambapo leo Jumatatu Oktoba 31 yameanza kufanyika mafunzo ya lugha ya alama kwa watoa huduma katika sekta za afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Chama Cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) mkoa wa Shinyanga.
Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku saba yamefadhiriwa na shirika la The Foundation For Civil Society kupitia mradi wa mafunzo ya lugha ya alama za msingi sekta za afya.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack aliwataka watoa huduma katika sekta za afya mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia muda mwingi kuwasikiliza watu wenye ulemavu wa kutosikia na kutoongea ili kuhakikisha kuwa watu hao wanapata huduma za afya kama wanavyopata watu wengine wasio na ulemavu.
Telack alisema watu wasiosikia na kuongea (viziwi) wamekuwa wakishindwa kupata huduma muhimu katika sekta za afya kutokana na vikwazo vya mawasiliano hivyo kuwataka watoa huduma waliopata mafunzo hayo kutumia muda wao mwingi kuwasaidia watu hao.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha 25 za matukio yaliyojiri leo Oktoba 31,2016
Wanachama wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoa wa Shinyanga ambacho sasa kina wanachama 544 tangu kilipoanzishwa mwaka 1990 kikiwa na wanachama sita pekee.
Mkalimani wakati wa mafunzo hayo ya lugha ya alama Prisca Mwakasendile akitoa maelezo kwa maneno na alama kwa wazungumzaji ukumbini ili kurahisisha mawasiliano na kuelewa mafunzo hayo,ambayo yamehudhuriwa na watoa huduma za afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Viziwi Tanzania mkoa wa Shinyanga.
Watoa huduma za afya kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Katibu CHAVITA mkoa wa Shinyanga Justine Shinday aliiomba serikali kupitia halmashauri za wilaya kuteua viongozi walau wawili watakaofanya kazi na CHAVITA kwa muda wote kama waajiriwa hali itakayowezesha asasi kuongeza ufanisi na ubora wa kuhudumia wanachama wake.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Ntuli Kapologwe alisema kupitia mafunzo hayo,watoa huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga watapata watajifunza lugha ya alama hivyo kuwasaidia kuhudumia watu wenye ulemavu wa kutosikia kuongea wanaofika kupata huduma za afya hospitalini.
Watoa huduma za afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Kushoto ni Emmaculatha Mihangwa,ambaye ni mwanachama wa CHAVITA mkoa wa Shinyanga akisoma risala ambapo pamoja na mambo mengine alisema viziwi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto lukuki na kusababisha wakose huduma muhimu zinazoathiri maisha yao hivyo ni vyema watoa huduma katika sekta muhimu na nyeti kama sekta ya afya wakafundishwa namna ya kuwasiliana na viziwi.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Katibu CHAVITA mkoa wa Shinyanga Justine Shinday akitoa elimu ya lugha ya alama ambapo alisema mafunzo hayo yawasaidia watoa huduma katika sekta za afya kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kutosikia na kuongea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea na mafunzo ya lugha ya alama
Mafunzo yanaendelea
Mafunzo yanaendelea ukumbini
Washiriki wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Mafunzo yanaendelea
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia somo ukumbini
Picha ya pamoja,washiriki wa mafunzo ya lugha ya alama na mkuu wa Shinyanga Zainab Telack
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin