Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Video : MSANII NYANDA MADIRISHA AMEFUFUKA??? AU NI UONGO??



Mr Bicon

Nyanda Madirisha enzi za uhai wake


Kuna uvumi kuwa msanii wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha “The Super Star” amefufuka.


Kufuatia uvumi huo uongozi wa Bicon Studio uliokuwa unafanya kazi na Nyanda Madirisha enzi za uhai wake,umeamua kutoa toleo maalum la video kuhusu kukanusha uvumi kuwa Nyanda Madirisha amefufuka baada ya kufariki dunia kwa ajali ya pikipiki Agosti 06,2016 akijiandaa kufanya show mkoani Simiyu.


Mkurugenzi wa Bicon Studio inayojuhusisha na uzalishaji wa kazi za wasanii wa nyimbo za asili iliyopo Kahama mkoani Shinyanga Emmanuel Nassor maarufu "Mr Bicon" ameandaa toleo maalum kukanusha uvumi huo.

Mr Bicon amefanikiwa kupata sauti za watu waliojirekodi na kuigiza sauti ya Marehemu Nyanda Madirisha akihojiwa radio Kahama.

Tazama Video hapa chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com