UMOJA
wa Vjana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umelihimiza Jeshi la polisi
nchini kutambua kuwa ujambazi, wizi wa kutumia silaha na uporaji bado ni
tatizo linalohitaji kushughulikiwa kwa nguvu zote kama ambavyo nchi
ilisimama na kutekeleza operesheni mbalimbali za ukombozi.
Pia,
umesisitiza kuwa usalama wa raia na mali zao unahitaji kulindwa ili
kuepusha vifo, hasara, unyang’anyi wa mali na vilema vya maisha kutokana
na matukio yanayoweza kuwakumba wasio na hatia mijini na vijijini.
Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alieleza hayo jana
alipomtembelea kumjulia hali majeruhi Said Ally, Mabibo Hostel.
Saidi
alijeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwa ni pamoja na
kutobolewa macho katika tukio wizi wa kutumia silaha Buguruni mjini Dar
es Salaam, Septemba mwaka huu.
Shaka
alisema tatizo la uhalifu, unyang’anyi, uporaji na ukwapuaji mali kwa
kutumia nguvu na silaha, linahiaji kutazamwa kwa kina na upana
unaostahili na vyombo vyenye dhamana vinavyosimamia usalama wa raia na
mali zao.
Alisema
kuna haja ya polisi kubuni mbinu mpya za kukabiliana na makundi ya
wezi, waporaji na majambazi kabla hawajaleta madhara na hasara kama
ilivyomtokea Said ambaye sasa amesababishiwa ulemavu wa kudumu wa
kutoona.
“Kila
siku mbinu za uhalifu, ujambazi, wizi wa kutumia nguvu na silaha
hubadilika, jukumu la kupambana na matukio hayo hatari ni la polisi kwa
kushirikiana na raia wema, janga hili likiachwa wananchi wataishi kwa
mashaka na hawatajituma kujiletea maendeleo,”alisema Shaka.
Alisema
ikiwa wananchi wanajituma kwa bidii kutafuta fedha na kubuni miradi ya
kiuchumi halafu majambazi na wanyang’anyi wanapora na kumfilisi
aliyetafuta ndani ya saa chache, hilo linaweza kuwatia hofu mwananchi na
wajasiriamali na kuwafanya washindwe kujituma kikamilifu jambo ambalo
litakuwa na madhara makubwa katika kuzalisha mali na kukuza uchumi.
Akizungumza
kwa masikitiko na huzuni kubwa , Shaka alisema tamaa ya kupata utajiri
kwa njia haramu kwa mtu mmoja mmoja au kikundi, kumemsibaishia hasara ya
maisha dhidi ya Said ambaye kwa sasa amekoseshwa uwezo wa kuendelea
kupiginia maendeleo yake ya kiuchumi na taifa kwa ujumla.
“Ifike
mahali tatizo la uhalifu, ujambazi na uporaji lishughulikwe kama
harakati za mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi, ukoma na
kifua kikuu, tukilipuuza tatizo hili litaigharimu jamii na kuwaletea
kadhia ya umasikini wananchi na Tanzania kwa ujumla,”alieleza.
Kwa
upande wake majeruhi Said aliishukuru UVCCM kwa kuonyesha kumjali na
kufika kumjulia hali kutokana na janga lililomkuta na kumpa msaada huku
akiwahimiza waendelee kuikumbusha serikali isimuache kwa sababu
amedhulumiwa utu wake na watu aliowatuhumu kuwa ni majambazi bila ya
hatia wala kosa lolote.
Said
alisifu ujio huo wa ujumbe kutoka Makao Makuu ya UVCCM Taifa
ulioongozwa na Shaka, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Omar
Matulanga na makatibu wa umoja huo kutoka wilaya tano za mkoa huo.
Alisema
akiwa kijana amefarijika kutembelewa na vijana wenzake huku akiwahimiza
wasimchoke kwa sababu sasa amekuwa kipofu na hajimudu tena kimaisha.
“Endeleeni
kuikumbusha serikali yetu na wasamaria wema wasinisahau, nina nguvu,
akili na maarifa ya kujituma ili nizalishe ila nimedhulumiwa macho yangu
na sina hakika kama nitaona kama mwanzoni “alisema