Basi lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kwenda jijini Dar es salaam, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement lenye namba zake za usajili namba ya usajili 534 BYJ jioni ya leo Jumapili October 30 2016.
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa na kuna taarifa kuwa mali zote zilikowemo katika
basi vimeteketea kabisa kwa moto.
Lori likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto
Baadhi ya Wakazi wa eneo la Kimara Stop Over na Kimara Suka wakielekea kushuhudia eneo la ajali kati ya basi la Safari Njema na Lori lililokuwa limebeba shehena kubwa ya mifuko ya Cement.
Baadhi ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza kuondoka na mifuko ya Cement iliyokuwa imebebwa na lori hilo.
Angalia video hapa chini Basi la Safari Njema likiteketea kwa moto
Social Plugin