Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIDEO YA WALIMU WAKIMSHUSHIA KIPIGO MWANAFUNZI OFISINI YAZUA GUMZO MTANDAONI,WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA ATOA KAULI


Video hii ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia leo alfajiri inawaonyesha walimu wakichangia kumpiga mwanafunzi mmoja ndani ya ofisi.



Walimu hawa wanaonekana si tu wanampiga mwanafunzi huyo kwa viboko, bali wengine wanampiga makofi ya uso, huku walimu wengine wakiwasihi wamuache mwanafunzi huyo kwani wanaweza kumuumiza.





Kuna hii taarifa mtandaoni katika ukurasa wa Facebook wa waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba


"Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo. 


Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian , darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndipo walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga .

Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza  na ndiye  aliyechukua video.

Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.

Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo
MWIGULU Nchemba, W MNN "



Tazama Video hapa chini walimu wakimshambulia mwanafunzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com