Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90
kuanzia jana (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka
wa masomo 2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa
hawajaridhishwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.
Serikali
imetenga Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi
119,012 – kati yao, wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na
wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi
20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea
rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management
System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari 31, 2017.
“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni kuingia katika mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na
kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake
ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa barua kwa ajili ya
sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.
ANGALIZO: Ada
ya Maombi ya Tshs 10,000/- iliyopaswa kulipwa na waombaji mikopo kwa
MPesa kwa ajili ya malipo ya Rufaa (HESLB) imefutwa.Taratibu nyingine
zinabaki palepale
Social Plugin