Emmanule Ntobi |
KUHUSU KUJIUZULU UJUMBE WA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA KWA MHE. DAVID NKULILA DIWANI WA CCM, KATA YA NDEMBEZI.
Heshima yenu wakuu,
Nimepokea simu na ujumbe mbalimbali kutaka nitoe tamko langu, iko hivi;
Binafsi na kambi ya Madiwani Upinzani Manispaa ya Shinyanga, Nimepokea kwa msituko mkubwa taarifa ya kujiuzulu UJUMBE wa Kamati ya Fedha na Utawala Manispaa ya Shinyanga.
Ifahamike kuwa, Kamati ya Fedha na Utawala, huundwa kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Manispaa za 2013, ambapo wajumbe wake 5 huingia kwa nafasi zao. Ila wajumbe 2 huchakuliwa kwa kupigiwa kura na Baraza zima la Madiwani.
NINI TAFSIRI YAKE.
Ni kuwa Mhe. Nkulila hakuteuliwa na Meya wala Mkurugenzi, kama zilivyo TAMATI zingine bali ALICHAGULIWA na Madiwani na tulimpigia kura kuwa ni mjumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala.
Pia, nakumbuka siku ya uchaguzi wa Mhe. Nkulila kuwa Mjumbe wa kamati ya Fedha na Utawala, Tarehe 10.12.2015 kulikuwa na mizenge sana. Lakini kama CHADEMA tulimuona anafaa kwa ajli ya "CHECK & BALANCE"
Kambi yetu ya Upinzani CHADEMA tulimuhitaji sana, ili awe Mjumbe wa kamati ya Fedha na Utawala.
Ifahamike pia, Kamati ya Fedha na Utawala ni kamati Nyeti kuliko zote katika ustawi wa Halmashauri zetu Nchini.
Hivyo, Kati ya Madiwani wa maCCM Manispaa Shinyanga, Mhe. Nkulila ni tofauti na madiwani wa MaCCM wengine, Naweza sema ni Mtu Jasiri, Mkweli na Mwenye msimamo Mkali dhidi ya dhuruma, Haki na Usawa wa wananchi wake na Manispaa kwa Ujumla.
Tofauti na Mhe. Nkulila, Madiwani wangine wa CCM na Baadhi yao ni wapiga dili, na wala RUSHWA wakubwa tofauti na Mhe. Nkulila David. Wengi wao wamepitisha suala la Greda ambalo manispaa timekula hasara ya zaidi ya Million 520. Wametetea sana haramu hiyo.
Kwa muktadha huo, nimesikitika na kusikitishwa sana kwa Mhe Nkulila kuamua kujitoa kwenye kamati ya Fedha na Utawala ambayo ni NYETI katika Halmashauri ya Manispaa.
Naam, Kama CHADEMA tumesikitika na Tumetikishwa kwa kuondoka kwa Mhe.Nkulila, Lakini Namkaribisha tuweze kupambana hata nje ya kamati ya Fedha na Utawala, tuhakikishe hakuna hata senti moja inafisadiwa na kuibiwa.
Viva Nkulila
Emmanuel Ntobi.
Diwani Chadema Ngokolo
Social Plugin