Kufuatia
kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia
(2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume ameweka wazi maneno matatu ya
mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito katika maisha.
Akizungumza
nyumbani kwa marehemu, Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni
mtoto wa kiume wa marehemu, alisema kuwa baba yake alitoa maneno matatu
ya kuukubali ukweli wa maisha baada ya Daktari kumueleza kuwa asingeweza
kupona.
“That’s life (hayo ndiyo maisha),”
Benjamin alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno
yake ya mwisho baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya
Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa
matibabu.
Maneo
ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote kuwa maisha huanza na huisha,
hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna aishie milele hivyo tuishi kwa
kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.
Sitta
ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na
viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi dume uliokuwa
ukimsumbua kwa muda mrefu.
Alitangaza
kustaafu siasa muda mfupi baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi
mkuu wa mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa msitari
wa mbele kumnadi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John
Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.
Benjamini
alieleza kuwa marehemu atazikwa Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba
ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo ndiyo inayoratibu mazishi
“Tumempoteza
baba na kiongozi ambaye tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala
mbalimbali, tutafuata yale aliyokuwa akituelekeza,” alisema Benjamini.
Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
Social Plugin