Svetlana Pankratova kutoka Russia, ndiye mwanamke anayeweka rekodi yakuwa mwanamke mwenye miguu mirefu kuliko wote duniani ikiwa na urefu wa futi 6.5.
Alizaliwa huko April 29, 1971 (miaka 45), mjini Volgograd, Russia. Ana mchumba anayefahamika kwa jina la Jack Gosnell lakini pia alisoma katika Chuo Kikuu cha Virginia Commonwelth.
Lakini mwanadada huyo alifurahisha wengi siku alipokutana na mtu mfupi kuliko wote duniani kwani tofauti za maumbile yao zilionekana haswa pale kijana huyo aliposimama katikati ya miguu ya mwandada huyo na kuwafanya wengi kufurahia kuwaangalia huku wakiwapiga picha.
Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Pingping kutoka Mongolia, ana urefu wa inchi 29.3 na aliingia katika rekodi za dunia 2008.
Pankratova anafurahia umaarufu alioupata kupitia miguu yake lakini kwa upande mwingine huwa hapendi anakumbana na changamoto ya wanaume wengi kukataa kusimama naye kwa madai kuwa ni mrefu sana kuliko wao lakini pia mara nyingi hukosa nguo za ndani pia suruali za kumtosha.
Social Plugin