Kesi
ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, inayomkabili Mbunge
wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless lema na mke wake Neema Lema (33),
imeshindwa kusikilizwa maelezo ya awali.
Hatua hiyo ni baada ya Mbunge huyo kukwama kuletwa Mahakamani toka Mahabusu kwa sababu zisizojulikana.
Kukosekana
kwa Mbunge huyo kuonekana Mahakamani, kulimlazimu Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Agustino Rwezile kutoa amri ya kutolewa
hati ya kumtoa Mahabusu mshitakiwa huyo na kumleta mahakamani hapo ili
kesi hiyo isikilizwe maelezo ya awali.
Hata
hivyo tangu amri hiyo itolewe saa nne asubuhi hadi saa saba mchana
mshitakiwa hakuweza kuletwa mahakamani hapo, licha ya mke wake kuwepo
mahakamani hapo.
Rwezile alimtaka wakili wa serikali kueleza sababu za kushindwa kumleta Lema Mahakamani wakati Mahakama imetoa amri.
Wakili
wa serikali Fotunatus Mhalila alisema mshitakiwa ameshindwa kuletwa
Mahakamani kutokana na sababu zisizozuilika , ila kwa sababu upelelezi
umekamilika aliomba Mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa hoja za
awali.
Majibu
hayo yalipingwa vikali na Wakili wa utetezi, John Mallya ambaye alitaka
kufahamu sababu za kutomleta Lema anazodai hazikuweza kuzuilika ni zipi na kwa nini zisitajwe mahakamani.
“Mheshimia hakimu hizo sababu zisizoweza kuzuilika ni zipi, Wakili wa seriali atueleze, tujue kama siyo amedharau mahakama licha ya kutakiwa kumleta mshitakiwa,” alisema.
Baada
ya hoja hizo kutolewa Hakimu Rwezile aliendelea kusisitiza hati ya
kumtoa Mahabusu itolewe ili aletwe Mahakamani leo katika kesi hiyo,
ambayo itasikilizwa hoja za awali.
Awali
katika kesi hiyo Godbless Lema na mke wake Neema, alisomewa mahitaka
kuwa kati ya Agosti 20 Mwaka huu ndani ya Arusha,walimtumia ujumbe wa
simu ya kiganjani Mkuu huyo wenye lugha ya matusi , huku wakijua ni kosa
kisheria.
Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulitumwa kutoka 076415**47 namba 075655**18 kwenda namba 0766-75**75 ukidai, “Karibu, tutakuthibiti kama Uarabuni wanavyothibiti mashoga.” Washitakiwa walikana shitaka hilo na walipatiwa dhamana
Social Plugin