Uongozi
wa Klabu ya Azam FC kwa masikitiko makubwa, unatangaza kifo cha
mwenyekiti wake, Mzee Said Mohamed Abeid, kilichotokea alasiri ya
Novemba 7, 2016, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Mzee
Said Mohamed, atakumbukwa kama mmoja wa nguzo muhimu kwenye mafanikio
ya klabu ya Azam FC tangu kuanzishwa kwake miaka takribani nane
iliyopita.
Chini
ya uongozi wake kama mwenyekiti wa Azam FC, aliiongoza klabu hii
kunyakuwa mataji mbalimbali makubwa na kwa mafanikio, ikiwemo taji la
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe
la Mapinduzi mara mbili pamoja na Ngao ya Jamii.
Si
hivyo tu, mchango wake Mzee Said Mohamed hauku-ishia nyumbani kwake
Azam FC tu, bali hata kwenye familia ya soka la Tanzania kwa ujumla wake
ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa ni makamu mwenyekiti wa bodi ya
ligi kuu Tanzania bara na mjumbe wa kamati mbalimbali za shirikisho la
soka Tanzania, TFF.
Sisi Azam FC, tutamkumbuka Mzee Said Mohamed kwa ucheshi wake, ukarimu na uchapakazi wake kwa ujumla.
Marehemu alizaliwa tarehe 20 Machi 1940 visiwani Zanzibar na anatarajiwa kuzikwa Jumanne leo
tarehe 8 Novemba, 2016 kwenye makaburi ya Kisutu baada ya swala ya
Alasir, mwili wake utaswaliwa kwenye msikiti wa Maamour Upanga.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake Said Mohamed Abeid mahali pema peponi, Amiin,
Innalilah Wa-inna-ilaih Rajioun.
Nassor Idrissa,
Makamu Mwenyekiti,
Azam Football Club.
Social Plugin