Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA SOKA KUTOKA BRAZIL YAANGUKA

Ndege iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense kutoka Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji wa Medellin nchini Colombia, mamlaka zimethibitisha.


Taarifa kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa watu 76 wamefariki dunia huku watano wakipona.


Maofisa wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Copa Sudemericana dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.


Kutokana na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com