Jumapili,November 06,2016- Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino) cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Afisa Mahusiano na Habari wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino Tanzania ,Josephat Torner amekabidhi msaada uliotolewa na marafiki zake kutoka Kampuni ya Safari nchini Israel walioguswa na changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ualbino katika nchi za Afrika.
Miongoni mwa misaada iliyotolewa na marafiki wa Josephat Torner kutoka nchini Israel ambako hivi karibuni alitembelea na kuwaeleza matatizo ya watoto wenye ualbino nchini Tanzania ni pamoja na nguo,viatu,miwani ya kuzuia mionzi ya jua na mafuta ya kuzuia mionzi ya jua.
Vifaa hivyo ni kwa ajili ya watoto wanaoishi katika kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga,kituo cha Malangale mkoani Rukwa,shule ya msingi Mapinduzi mkoani Katavi na vingine vitapelekwa mkoani Arusha vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni nne na laki nane( Mil 4.8).
Akikabidhi vifaa hivyo katika kituo cha Buhangija,Torner amesema vifaa hivyo vimepatikana baada ya kuwaeleza rafiki zake wa Israel kuhusu changamoto zinazowakabili watoto wenye ualbino.
“Rafiki zangu wa Israel wamenituma kuwafishieni msaada huu,lakini pia wameahidi kuendelea kutoa misaada mbalimbali ili kupunguza na hata kumaliza kabisa changamoto zilizopo katika vituo vya kulelea watoto wenye ualbino”,alieleza Torner.
Kwa upande wake mwalimu mlezi wa watoto katika kituo cha Buhangija ambacho kinalea watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasiosikia na wasioona, Jackson Leonard aliwashukuru watu wa Israel kwa kuona umuhimu wa kusaidia watoto hao huku akitoa wito kwa watu wengine wenye mapenzi mema kuendelea kuwasaidia watoto hao.
Mwandishi wetu,Kadama Malunde,alikuwepo katika kituo cha Buhangija ametusogezea picha 30,matukio yaliyojiri
Mwalimu mlezi wa watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyang Jackson Leonard akimkaribisha
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania ,Josephat Torner
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino Tanzania ,Josephat Torner (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa kukabidhi msaada uliotolewa na marafiki zake kutoka nchi ya Israel
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania ,Josephat Torner akikabidhi nguo kwa kijana mwenye ualbino katika kituo cha Buhangija,baada ya kumkabidhi miwani ya kuzuia mionzi ya jua
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akikabidhi nguo mtoto mwenye ulemavu wa kusikia.Katikati ni katibu wa Chama cha Albino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anaeli
Kulia ni Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akifurahia baada ya kumkabidhi miwani kijana mwenye ualbino
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akikabidhi nguo baada kukabidhi miwani
Kulia ni Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akifurahia baada ya kumkabidhi miwani kijana mwenye ualbino
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akikabidhi nguo baada kukabidhi miwani
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akiendelea kukabidhi nguo na miwani
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akiendelea kukabidhi nguo
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akimvalisha miwani kijana mwenye ualbino
Zoezi la kukabidhi nguo na miwani linaendelea
Pokea zawadi kijana
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akiangalia miwani ili kumkabidhi mtoto mwenye ualbino aliyekuwa amebeba mtoto mwenye ualbino mgongoni
Naangalia miwani ya kukufaa......
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa amevaa miwani
Zoezi la kukabidhi nguo linaendelea
Mwalimu mlezi wa watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyang Jackson Leonard akimkabidhi nguo mtoto
Nakukabidhi nguo hii.....
Kijana akiwa amevaa miwani
Zoezi la kukabidhi nguo linaendelea
Watoto wakisubiri zawadi....
Zoezi la kugawa kofia likachukua nafasi
Kijana akiwa amevaa kofia
Kijana mwenye ulemavu wa kutoona akipokea zawadi ya nguo
Kushoto ni Afisa Mahusiano na Habari wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino Tanzania, Josephat Torner akiwa na baadhi ya watoto wenye ualbino wakiwa wamevaa miwani ya kuzuia mionzi ya jua
Watoto wakiwa wamevaa miwani
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akimpa zawadi ya mfuko mtoto mwenye ualbino
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akimpa zawadi ya pochi mtoto ulemavu wa kutosikia
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akiwa na watoto
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania , Josephat Torner akiagana na watoto.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin