Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: TPDC YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA,YATOA ELIMU KUHUSU MAFUTA NA GESI


Alhamis,Novemba 03,2016 katika ukumbi wa St.Dominic jijini Mwanza.Pichani ni Meneja Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka kanda ya ziwa (Mwanza,Geita,Mara,Kagera na Shinyanga) kuhusu masuala ya gesi na mafuta ukiwemo mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga nchini Tanzania-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Msellemu alisema lengo la mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania-TPDC ni kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari kuhusu Gesi na Mafuta ili waweze kuandika habari sahihi ukiwemo mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania

 Meneja Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu alisema mafunzo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa waandishi wa habari na kuwawezesha kuandika habari kwa usahihi zaidi.


Aliyesimama ni mgeni rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Kombe Danty aliyemwakilisha mkuu wa wilaya hiyo Maria Tesha Onesmo akifungua semina hiyo.
Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Kombe Danty aliwataka waandishi wa habari wa habari kutumia elimu waliyopewa kuandika habari sahihi kuhusu bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.Kushoto ni Meneja mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu.Kulia ni Mwanasheria kutoka TPDC John Mgayambasa

Mwanasheria kutoka TPDC John Mgayambasa akielezea kuhusu bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania

Mwanasheria kutoka TPDC John Mgayambasa akisisitiza jambo ukumbini

Mhandisi wa Petroli kutoka TPDC,Koleta Selsi akizungumzia kuhusu maendeleo ya sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini Tanzania

Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja ya mkoani Shinyanga,Simeo Makoba akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini

Afisa Uhusiano kutoka TPDC Augustino Kasale akifafanua jambo ukumbini
Afisa Uhusiano kutoka TPDC Augustino Kasale akifafanua jambo ukumbini





Waandishi wa habari wakiwa ukumbini


Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Mafunzo yanaendelea

Mafunzo yanaendelea




Mafunzo yanaendelea



Aristides Robert kutoka TPDC akielezea matumizi ya gesi asilia
Maafisa kutoka TPDC


Picha ya pamoja washiriki wa semina hiyo na mgeni rasmi
Picha ya pamoja washiriki wa semina hiyo

Picha ya pamoja
 -Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com