Kufuatia kutangazwa kwa Donald Trump kuwa rais mteule wa Marekani, wananchi wa Marekani wameandamana katika miji saba kupinga ushindi huo wa Trump.
Waandamanaji hao wamekusanyika nje ya mnara maarufu wa Trump ‘ Trump Tower’ mjini New York wakipaza sauti za kumpinga Trump. Wengine walionekana nje ya Ikulu ya Marekani wakipaza sauti kuwa “Not my president” (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.
Wengi wa waandamanaji walioongea na CNN wameelezea kuwa wana wasiwasi sana kuhusu Trump kwa vile kuongoza Marekani sio kama kuiongoza nchi yoyote duniani.
Social Plugin