Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Kanegere kata ya Bukandwe wilaya ya Mbongwe mkoani Geita.
Ajali hiyo imetoa Jumamosi Desemba 24,2016 majira ya saa 9 alasiri.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema miongoni mwa watu waliofariki ni padri wa kanisa katoliki jimbo la Kahama mkoani Shinyanga Andrew Lupondya aliyekuwa anaendesha gari na kubeba waumini ambao baadhi yao wamefariki dunia.
Kaimu mganga wa hospitali ya wilaya ya Mbogwe,Salum Ndimu amekiri kupokea miili minne ya marehemu na majeruhi
Social Plugin