Jumamosi Desemba 03,2016- Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameendelea na ziara ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu masuala ya ardhi.
Leo ilikuwa ni zamu ya wananchi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga yenye kata 25,vijiji 117 na vitongoji 660.
Akizungumza katika viwanja vya Ushirika katika mji wa Mhunze wilayani Kishapu wakati akisikiliza kero za ardhi kutoka kwa mwananchi mmoja baada ya mwingine,Waziri Lukuvi alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli imedhamiria kumaliza kero za ardhi.
Ziara hiyo imekuwa na manufaa kwa wakazi wa Kishapu baada ya waziri huyo kuahidi kuanzisha baraza la ardhi katika wilaya hiyo hivi karibuni wiki ijayo atateua mwenyekiti wa baraza hilo ili kutatua kero za ardhi na kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika wilaya ya Shinyanga.
Lukuvi aliwataka maafisa wa ardhi nchini kushirikiana na sekta binafsi kupanga miji na wao kubakia kuwa wasimamizi wa taratibu zote kwani serikali haina uwezo wa kuajiri maafisa ardhi na mipango miji wengi.
Waziri Lukuvi pia amepiga marufuku vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wawekezaji wasio waaminifu waliopewa vibali vya kuchimba madini kuwahamisha wananchi katika maeneo ya uchimbaji bila kuwalipa fidia.
“Kama umepewa kibali na serikali cha kuendeleza eneo flani la mgodi wale wananchi wa pale lazima waondoke lakini waondolewe kwa heshima,wapewe fidia inayofanana na thamani ya mali zao zilizopo eneo lenye mgodi siyo fidia ya kupunza wananchi ”,alisema Lukuvi.
Tazama Matukio katika picha wakati wa ziara ya Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wilayani Kishapu Desemba 03,2016.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akisalimiana na maafisa wa serikali wilayani Kishapu baada ya kuwasili katika wilaya hiyo.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliyekuwa anamwakilisha mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba
Aliyesimama ni kaimu mkuu wa wilaya ya Kishapu Josephine Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga akimkaribisha Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi(mwenye shati jeupe) akiingia katika jengo la halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kukutana na wakuu wa idara hususani sekta ya ardhi katika wilaya ya Kishapu kabla ya kwenda katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika mji wa Mhunze
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi(katikati) akizungumza na wakuu wa idara katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu.Kulia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Kishapu Josephine Matiro,kushoto ni katibu tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Jumanne Chaura akisoma taarifa ya sekta ya ardhi wilaya ya Kishapu ambapo alisema idara hiyo ina watumishe 7 pekee huku akibainisha migogoro mbalimbali ya ardhi ukiwemo wa mpaka wa wilaya ya Kishapu na Igunga unaosababishwa na kugombania mto uliopo eneo hilo
Maafisa mbalimbali waliokuwa wameambatana na waziri katika ziara hiyo wakiwa ukumbini.Wa pili kutoka kulia ni meneja wa Shirika la nyumba la taifa (NHC) mkoa wa Shinyanga Ramadhan Macha
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza baada ya kupokea taarifa ambapo aliwataka maafisa ardhi kuhakikisha kuwa wananchi wanapewa hati za ardhi na nyumba
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiendelea kuzungumza na wakuu wa idara
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alishauri maafisa wa ardhi kuwa na utaratibu wa kupanga miji ili kutoa fursa za kutangaza miji yao
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi vitabu vyenye muongozo namna ya kupanga miji sambamba kitabu chenye majina 33 ya makampuni yaliyojitolea kushirikiana na serikali kupima ardhi bila serikali kutoa gharama yoyote
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Jumanne Chaura akipokea vitabu hivyo
Aliyesimama ni kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ferdinand Mpogomi akimweleza waziri kero ya kukosekana kwa baraza la ardhi katika wilaya ya Kishapu
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa Kishapu katika mji wa Mhunze kabla ya kuanza kupokea kero za ardhi zinazowakabili wananchi
Wananchi wakiwa eneo la mkutano wakisubiri zamu ya kueleza kero za ardhi kwa waziri
Mkazi wa Kishapu Sakina Magezi akieleza kero yake kwa waziri wa ardhi
Mkazi wa Kishapu Daudi Amos akieleza kero ya kutolipwa fidia eneo lake lililochukuliwa na halmashauri
Bwana Daudi Amos akikabidhi vielelezo muhimu vya madai yake kwa waziri
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa maelekezo kwa mthamini wa wilaya ya Kishapu Reuben Lauwo (mwenye shati ya bluu) na afisa ardhi wa wilaya ya Kishapu Grace Pius (katikati) kumlipa fidia bwana Daudi Amos
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo
Waziri Lukuvi akifafanua jambo kwa wananchi
Waziri Lukuvi akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kulipwa fidia za maeneo yao kwa mujibu wa sheria siyo kuwaondoa kienyeji na kuwalipa malipo yasiyostahili
Kaimu mkuu wa wilaya ya Kishapu Josephine Matiro akiteta jambo na katibu tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese
Wananchi wakifualia kilichokuwa kinaendelea
Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwahamasisha wakazi wa Kishapu kulipia kodi za nyumba/viwanja na wenye mashamba kuhakikisha wanayapima
Mkutano unaendelea
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao
Mkazi wa Kishapu akielezea kero yake kwa waziri
Waziri Lukuvi akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kutoogopa kuwafichua watu wanaochangia kuwepo kwa migogoro ya ardhi huku akiwataka watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanapima viwanja vingi kuliko mahitaji ya wananchi
Kaimu mkuu wa wilaya ya Kishapu Josephine Matiro akizungumza baada ya waziri Lukuvi kumaliza kusikiliza kero za wananchi
Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ferdinand Mpogomi akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa kusikiliza kero za wananchi wa wilaya ya Kishapu.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin